Jumanne 9 Juni 2026 - 12:41
Kukumbuka kuwa dunia inaisha humwacha mwanadamu huru kutokana na kushikamana nayo kupita kiasi

Hawza/ Kiongozi shahidi wa Mapinduzi akirejelea hadithi: «لِدْ لِلْمَوْتِ وَاجْمَعْ لِلْفَنَاءِ وَابْنِ لِلْخَرَابِ», alisisitiza kwamba; kila kitu ambacho mwanadamu hukikusanya duniani hatimaye kitatoweka. Kwa maelezo yake, kuzingatia ukweli huu husababisha kupungua kwa kushikamana na dunia na humkumbusha mwanadamu mwisho wa mambo kabla ya kuanza kila hatua.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Shahidi Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu aitakase nafsi yake tukufu), mwanzoni mwa vikao vya masomo yake ya juu ya fiqhi (Dars Kharij), alikuwa akifafanua hadithi za kimaadili.

"Katika dunia hii hakuna kitu cha kudumu" ni maudhui ya ufafanuzi wa hadithi ya kimaadili kutoka kwa Mtume mtukufu wa Uislamu, Muhammad Mustafa (saww), ambapo matini yake imechapishwa kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.

Katika kitabu cha Al-Kafi, imepokewa kutoka kwa Imam al-Baqir (as):

"Kila siku mnadi hunadi: Ewe mwana wa Adam! Zaliwa kwa ajili ya kufa." (1)

Huu ni ukweli ulio wazi ambao mara nyingi akili na fikra za watu hughafilika nao; kwamba kila kuzaliwa mwishowe kunaelekea katika kuangamia na kutoweka.

وَاجْمَعْ لِلْفَنَاءِ

"Na kusanya kwa ajili ya kuangamia."

Kusanya: fedha, mali, vitu, vitabu, vifaa vya maisha unavyovitamani kwa upande wa mambo ya kimada na yanayoonekana, mamlaka na mengineyo. Jitahidi kukusanya yote hayo, lakini ni kwa ajili ya kutoweka.

Vyote hivyo vitatoweka.

Kila tunachokusanya kitaangamia, kwa muda mfupi tu huwa kigeni kwetu au sisi huwa wageni kwacho; wakati mwingine hicho kitu hubakia nasi tunaondoka, lakini nacho pia baada yetu kitaondoka.

وَابْنِ لِلْخَرَابِ

"Na jenga kwa ajili ya kubomoka na kuharibika."

Huku ni kutukumbusha kuhusu asili ya ulimwengu huu; ulimwengu wa kupita na ulimwengu wa kimada, ambapo kila kitu katika dunia hii ni kwa ajili ya kuja na kuondoka; hakuna kitu chenye kubakia milele.

Mwanadamu anapaswa kulitilia maanani jambo hili na kulielewa, anatakiwa kuukumbuka mwisho wa jambo wakati analianza jambo hilo, hili ni funzo kwetu.

Hupunguza kushikamana kupita kiasi; iwe ni kushikamana na vitu na mali zinazohusiana nasi, au kushikamana mno na nafsi zetu wenyewe.

(1) Ash-Shafi, uk. 876.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha